Mitaala ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu imewekwa katika tovuti hii.
Mitaala
hii ni ile iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka
2005 ambayo ilizingatia ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa
maana badala ya ule wa awali unaozingatia maarifa. Mitaala hii imekuwa
ikitumika kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa.
Mitaala
imeboreshwa kufuatia mchakato wa majadiliano katika vikao vya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyofanyika mwezi Februari 2013,
pamoja na maoni na hoja mbalimbali zilizotoka kwa wadau wa elimu.
Pamoja
na maboresho yaliyofanyika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inaweka mitaala hii wazi kwa wadau wote wa elimu na jamii kwa ujumla ili
kuendelea kupata maoni zaidi ya jinsi na namna ya kuiboresha mitaala
hiyo.
Aidha, katika kipindi hiki cha kukusanya maoni, mitaala hii itaendelea kutumika hadi hapo mchakato wa kuihuisha utakapokuwa umekamilika. BOFYA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI
No comments:
Post a Comment